Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron anatarajiwa kutangaza katika mkutano wa kupinga ufisadi kwamba makampuni ya ng'ambo yanayomiliki mali London yatalazimishwa kujisajili wazi wamilki mali hiyo.
Hatua hiyo imeundwa imeidhinishwa kuzuia wafisadi na nchi dhidi ya kuhamisha, na kuficha fedha kupitia soko la London. Nchi kadhaa nyengine huenda pia zikaahidi kuidhinihsa usajili wa wamilki asili wa makampuni.
Kuna takriban kampuni 100,000 England pamoja na Wales zinazomilikiwa na makampuni ya nje nyingi zikiwa mjini London.
Zina thamani ya mamilioni ya pauni na nyingi hutumiwa kuficha fedha ambazo zimepatikana kwa njia za kifisadi.
Katika siku zijazo kampuni yoyote itakayo taka kununua au kumiliki mali ni lazima ijisajili.
Baadhi ya maenoe ya Ukngereza na milki zake zitajiunga nchi nyingine 33 katika kukubali kudhirisha usajili wa wamilki kampuni, taarifa zinazopaswa kuwa wazi kwa polisi .
Kutakuwa na kituo cha ushirikiano cha kukabiliana na ufisadi London na hatua kubwa zitachukuliwa dhidi ya wakuu wanaoshindwa kuzuia udanganyifu au ulanguzi wa fedha katika kampuni zao.
Mtihani wa mpango wa waziri mkuu Cameron utakuwa ni nchi ngapi nyingine zitakazofuata mfano huo.
Kwa mfano Virgin Islands haihudhirii mkutano huo na haijakubali kutoa taarifa zozote kuhusu kampuni zilizoko huko