WATU wanaodhani kuwa majambazi wamewauwa watu 8 wa familia tatu na kuiba vyakula kijiji cha Mabatini kata ya Mzizima Amboni nje kidogo ya jiji la Tanga kisha kutokomea katika Mapango ya Amboni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo , Kamanda wa Polisi Tanga, Leonard Poul, alisema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na kuahidi kuwatia mbaroni majambozi hao.
Amesema katika matukio ya ujambazi mfululizo yanayojitokeza Tanga, jeshi la polisi kwa kushirikiana na vikosi vya Jeshi la Wananchi (JWTZ) na vyombo vya usalama wa Taifa watahakikisha waliofanya unyama huo wanafikishwa katika vyombo vya sheria.
Alisema tukio hilo lilifanyika usiku wa saa 7 na majambazi hayo kuingia nyumba moja baada ya nyengine na kufanya wizi wa vyakula katika maduka na kisha kuwauwa watu waliokuwa wamelala.
Alisema majambazi hayo yaliyokuwa na mapanga, visu na silaha nyenine za jadi walikuwa kundi ambalo idadi yake hakulitaja na kuingia nyumba mmoja baada nyengine kati ya nyumba tatu ambazo wamefanya unyama wao.
Alisema anaamini majambazi hayo ni masalia ya majambazi ambayo yalifanya vitendo vya uporaji na mauji na kukimbilia Mapangoni hivyo jeshi hilo linazidisha msako na ulinzi kwa wananchi.
Amewata wananchi kutokuwa na hofu na badala yake wafanye kazi zao za kujiletea maendeleo kwani wataendesha msako usiku na mchana kuhakikisha inawatia mbaroni.
Amewataja waliouwawa kuwa ni, Issa Hassan (50), Mkola Hussein(40), Hamis Issa(20), Mikidadi Hassan(70) Mahmood (40), Issa Ramadhan (25) Kadiir na Salim ambao hawakujulikana majina ya baba zao