POLISI
mkoani Rukwa inawashikilia askari wake wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi
wilayani Nkasi, wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh
milioni 7.2 wamsaidie mtuhumiwa.
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa Rukwa, Leonce Rwegasira alitaja askari hao kuwa ni
Konstebo Filbert Ruhemeja na Konstebo Bahati Sengerema, ambao walikuwa
wakifanya kazi katika Kituo cha Polisi mjini Namanyere wilayani Nkasi.
Alisema
polisi inawafanyia uchunguzi wa kina askari wake wawili, wanaotuhumiwa
kwa kashfa ya kuomba rushwa ya Sh milioni 7.2 na iwapo watabainika
halitasita kuwatimua na kuwafikisha mahakamani.
Rwegasira
alisema hayo jana ofisini kwake wakati anazungumza na mwandishi wetu
alipotaka kujua ni hatua gani zilizochukuliwa dhidi ya polisi hao
kutokana na kuwepo kwa tuhuma hizo za kuomba na kupokea rushwa.
Alisema
askari hao wawili wa polisi, wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya
fedha kutoka kwa mtu mmoja ili wamsaidie katika shitaka linalomkabili.