MAMLAKA
ya Mapato Nchini (TRA) kwa mwezi uliopita imekusanya Sh.Trioni
1.035 ambayo ni sawa na asilimia 99.5 ya lengo kukusanya sh.trioni
1.040 .
Akizungumza
leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa
TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa katika makusanyo ya miezi 10 wameweza
kukusanya sh. Trioni 10.92 ambayo sawa na asilimia 99 ya lengo ya
sh.trioni 11.02 katika lengo la kipindi hicho.
Amesema
kuwa TRA imedhamiria kukusanya zaidi ya sh. Trioni 1.4 na kuvuka
lengo la mwaka wa fedha wa 2015/2016 katika miezi miwili ya kumaliza
mwaka wa fedha ambalo ni sh. Trioni 12.3.
Kidata
amesema kuwa TRA itaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha
inafikia lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2015 / 2016 licha kuwepo
kwa changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo.
Amesema
kuwa wananchi wamejua umuhimu wa kodi na kuanza kutoa ushirikiano
katika kudhibiti mianya ya magaendo, pamoja na kuziba mianya ya upotevu
wa mapato ikiwa katika usimamizi wa mifumo ya mlipa kodi kulipa kodi
anayostahili bila usumbufu wowote.