Polisi
wapatao 20 wa Uganda walokua zamu kumlinda kiongozi wa upinzani Kiza Besigye,
akiwa anashikiliwa nyumbani kwake Kaswangati wamekamatwa na maafisa wa usalama
wa nchi hiyo.
Vyanzo vya
kuaminika vya polisi mjini Kampala vikizungumza na Sauti ya Amerika, vinaeleza
kwamba polisi hao wanashikiliwa na kuhojiwa kuhusu jinsi Dk. Besigye alivyoweza
kutroroka kutoka nyumbani kwakena kuhudhuria mkutano na wafuasi wake wiki
iliyopita.
Hata hivyo
msemaji wa polisi Patick Onyango amekanusha habari hizo siku ya Jumamosi
alipozungumza na waandishi habari na kusema hawezi kutoa maelezo zaidi isipokua
kusisitiza kua polisi hao hawajakamatwa.
Dr Besigye
kwa wakati huu anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Moroto, baada ya
kukamatwa pale video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha anakula
kiapu kama rais wa wananchi wa Uganda.
Mwendesha mashtaka wa taifa
amemfungulia rasmi mashtaka ya uhaini kutokana na kitendo hicho