Wakazi
wa Kata ya Sombetini na Osunyai, katika jiji la Arusha leo wameandamana
kuifunga barabara mpya ya lami Sombetini, wakishinikiza kuwekwa matuta katika
bara bara hiyo baada ya kugongwa watu zaidi ya 10 ndani ya miezi miwili.
By Mussa
Juma,Mwananchi mjuma@mwananchi.co.tz
Arusha. c
Tukio
hilo, limesababisha usafiri wa magari ya abiria kusimama katika barabara hiyo
na kuzua tafrani kubwa kuanzia majira ya asubuhi hadi mchana walipofika
viongozi wa jiji, polisi na madiwani.
Akizungumza
katika eneo hilo, Diwani wa Kata ya Sombetini, Ally Benanga alisema, wananchi
wa eneo hilo, wameshoshwa na vifo lakini, tayari walitoa malalamiko na baraza
la madiwani liliagiza jiji kuweka matuta.
"kikao
cha madiwani kilifikia agizo la kuwekwa matuta sasa tunataka kazi hii
kufanyika" alisema
Meya wa
jiji la Arusha, Calist Lazaro aliagiza uongozi wa jiji ndani ya siku tano,
kuweka matuta katika barabara hiyo na alama zote za barabarani.
"Hatuwezi
kuvumilia watu kugongwa kutokana na barabara hii, kukosa alama za barabarani na
matuta sasa kama tulivyoagiza madiwani tunataka ijengwe''alisema.
Jane
Maeda mkazi wa Sombetini, alisema takriban kila wiki mtu mmoja anagongwa
sambamba na watoto wa shule hivyo ni bora barabara waifunge ili kuepusha maafa
zaidi.
Baada ya
majadiliano baina ya wananchi, Meya na madiwani wa kata hizo, mbili hatimaye
wananchi walikubali kutoa mawe waliyoweka barabarani na barabara kupitika.
Mhandisi
wa jiji Gaston Gasana ameeleza barabara hiyo, itawekewa matuta na alama za
barabarani kama ambavyo wamekubaliana katika siku tano kuanzia jana.